Mwanza Wazindua Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa.

  Mkoa wa Mwanza umefanya Uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji ambao umeandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF).

  Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella akitoa hotuba ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa huo uliondaliwa na ESRF kwa chini ya ufadhili wa UNDP katika hafla fupi iliyofanyika katika viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa jijini Mwanza.

  Mwongozo huo ni sehemu ya ripoti tatu zilizotokana na agizo la mkoa wa Mwanza la kutaka kuwekewa pamoja taarifa sahihi zinazogusa uwekezaji mkoani humo ili kurahisisha na kuwavutia wawekezaji wa ndani na nje.

  Ripoti nyingine ni Fursafiche katika Viwanda (Industrialization Potentials Report), na Ripoti ya Fursa za Uwekezaji (Investment Opportunities Report) .

  Akizungumza katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, Mashirika ya Umma, Sekta binafsi na mashirika ya kimataifa, Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella, alisema walilazimika kuwatafuta wataalamu wa ESRF, kuwasaidia kuweka pamoja fursa zote za mkoa katika mpangilio mmoja unaobainisha fursa zilipo.

  Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akitoa taarifa kuhusu uandaaji wa Mwongozo wa Uwekezaji mkoani Mwanza ulioandaliwa na taasisi yake katika hafla fupi ya uzinduzi wa mwongozo huo uliofanyika jijini Mwanza.

  Mkuu na Mtaalamu wa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Bw. Amon Manyama akitoa salamu za UNDP katika hafla fupi ya uzinduzi wa Mwongozo wa Uwekezaji wa mkoa wa Mwanza uliofanyika kwenye viwanja vya ofisi za Mkuu wa Mkoa huo jijini Mwanza.

  Alisema katika kukabiliana na changamoto hizo waliiomba Taasisi hiyo kufanya utafiti na uchambuzi wa kina ili kubaini fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa huo na ndio wakatoka na ripoti tatu ikiwa Mwongozo huo.

  Alisema kazi hiyo ilifanyika kwa miezi 4 kwa msaada wa kifedha kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kuanzia mwezi Julai 2017 hadi Novemba 2017.

  Mongela alisema: wawekezaji wamekuwa wakipata taabu namna ya uoanishaji wa taarifa zinazotolewa kwao kutoka mamlaka moja hadi nyingine.

  Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mh. John Mongella (wa tatu kulia), Mkurugenzi Mtendaji Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati), Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF Bi. Margareth Nzuki (wa pili kulia), Mkuu na Mtaalamu wa Miradi kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Tanzania, Bw. Amon Manyama (wa tatu kushoto), Mtafiti Mshiriki wa ESRF, Dkt. Hoseana Lunogelo (wa pili kushoto) Watafiti vijana kutoka ESRF Bw. Mussa Martine (kushoto) pamoja na Bw. Joseph Nyampepela Ngonyani (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakiwa wameshika nakala za Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoa wa Mwanza.

  Soma Zaidi

  Pekua Mwongozo wa Uwekezaji wa Mkoani Mwanza


  Last updated on 2017-11-29
ESRFs activities are supported by the Government of the United Republic of Tanzania, United Nations Development Programme (UNDP), African Capacity Building Foundation (ACBF) and International Development Research Centre (IDRC)