Prof. Brian Van Arkadie atoa somo kuhusu mapinduzi ya kilimo.

    Ingawa mazao hayo ya kilimo yameonakana kuporomoka kutoka miaka hiyo, kumekuwepo na ongezeko kubwa la pengo la kipato kati ya watu wa mijini na vijijini huku ukuaji wa vijijini ukikumbwa na udumavu. Pamoja na ukweli huo amesema profesa huyo, kuna mabadiliko ya kutosha katika maeneo ya vijijini na katika kilimo kwamba kusema hakuna maendeleo si kitu sahihi.

    Prof. Brain Van Arkadie ambaye ni msemaji mkuu wa mhadhara mkubwa ulishirikisha wanazuoni mbalimbali kujadili historia na nafasi ya kilimo na sera zake katika kufanikisha safari ya viwanda ya Tanzania, kwa kuangalia mazao ya chakula kama mazao ya biashara akiwasilisha utafiti wake katika mkutano huo ulioandaliwa na ESRF na kufanyika jijini Dar es Salaam.

    Alisema zipo sababu za kupungua kwa uzalishaji wa mazao makuu kama kahawa, tumbaku, mkonge na hilo linatokana na serikali kuingilia kati mfumo wa masoko ambao haukuwa unaswihi. Profesa huyo alisema hata hivyo, kwa miaka 50 kilimo cha Tanzania kimefanikiwa kulisha taifa kwa kuwezesha watu wa mijini na vijijini kupata vyakula hasa vile vya msingi ingawa wakati mwingine ukame ulileta usumbufu.

    Huku Tanzania ikiwa na ongezeko la watu kutoka milioni 12.3 kwa mwaka 1967 hadi milioni 44.9 kwa mwaka 2012 ni dhahiri ukuaji wa kilimo umesaidia kuiweka nchi katika hali bora zaidi ya upatikanaji wa chakula ingawa ifikapo mwaka 2030 watu wa mijini watakuwa wameongezeka kwa asilimia 37 na kuweka shinikizo ambalo kwa namna nyingine linaweza kuwa na maana kwa kuwa mazao ya chakula yatakuwa ndiyo ya biashara na hivyo kuacha kutegemea yale ya asili kama kahawa na tumbaku.


    Last updated on 2017-08-24
ESRFs activities are supported by the Government of the United Republic of Tanzania, United Nations Development Programme (UNDP), African Capacity Building Foundation (ACBF) and International Development Research Centre (IDRC)