ESRF yaendesha warsha ya fursa katika ufugaji samaki kibiashara.

  Watanzania wameshauriwa kuchangamkia fursa za ufugaji wa samaki kibiashara kutokana na kuwepo kwa soko kubwa la bidhaa hiyo huku mnyororo wake wa thamani ukiwa na uhai mrefu kisekta.

  Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Magreth Nzuki akitambulisha wageni na malengo ya warsha ya fursa za ufugaji Samaki kibiashara.

  Kauli hiyo imetolewa na Ofisa wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Bwana Amon Manyama wakati akifunga warsha ya siku moja juu ya ufugaji wa samaki kibiashara iliyofanyika katika viwanja vya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na watu takribani 400.

  Makamu Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji Viumbe Hai Majini wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Ritha Maly akisoma hotuba ya kufungua warsha ya fursa za ufugaji samaki kibiashara.

  Bw. Manyama alisema kwamba watanzania wasipotumia fursa ya ufugaji wa samaki baada ya miaka mitano watakuwa wamepoteza fursa hiyo adimu inayoshawishi viwanda vidogo na vya kati. Alisema kimsingi yeye anaamini sekta ya ufugaji wa samaki ni viwanda tosha kutokana na muingiliano wake huku watu wakinufaika na minofu pia kuna ngozi na magamba ambayo yanakazi kubwa ya kutengeneza urembo, viatu na kadhalika.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akisoma hotuba ya ukaribisho katika warsha ya fursa za ufugaji samaki kibiashara.

  Warsha hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)- Kitengo cha Maarifa na Ubunifu ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA)- Idara ya Sayansi ya Wanyama, Ukuzaji Viumbe Majina Nyanda za Malisho, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) – Kikosi cha Kambi la Rwamkoma pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) ilifunguliwa na Bi. Ritha Maly Kaimu Mkurugenzi Idara ya maendeleo ya viumbe wa majini.

  Baadhi ya washiriki wa warsha ya fursa za ufugaji samaki kibiashara wakipewa maelezo kuhusu ufugaji samaki kwa kutumia matanki.

  Akifungua warsha hiyo, Bi Ritha aliwashukuru waandaaji wa warsha hii kwa sababu ya uhitaji mkubwa wa samaki “Warsha hii imekuja wakati muafaka ambapo uhitaji wa samaki umeongezeka sana ukiambatana na changamoto za upatikanaji wa samaki wa kutosha hivyo uwepo wa fursa hizi zitakazowasilishwa leo zitakua hakika ni mkombozi mkubwa kwa kukuza uzalishaji wa samaki nchini na kufungua fursa za biashara ya samaki kwa kufanya ufugaji huu kibiashara.” alisema.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon Manyama na Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu ya Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Margareth Nzuki.

  Soma Zaidi

  Pakua/Download Mawasilisho/Presentations


  Last updated on 2017-07-24




ESRFs activities are supported by the Government of the United Republic of Tanzania, United Nations Development Programme (UNDP), African Capacity Building Foundation (ACBF) and International Development Research Centre (IDRC)