ESRF yaandaa mkutano kujadili biashara na uwekazaji kati ya Tanzania na China.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba kwa niaba ya Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango ametaka kuwapo na uratibu wenye maslahi mapana katika biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China.

  Alisema hayo wakati akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China.

  Aliwataka washiriki wa mkutano huo wa mwaka kujadili kwa makini namna ya kuratibu vizuri vitega uchumi na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili.

  Alielezea kufurahishwa kuwapo na mada mbalimbali zinaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China na kusema mada hizo zitumike vyema kuweka misingi mizuri yenye manufaa kwa pande zote mbili.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.

  Aidha aliipongeza ESRF kwa kuona haja ya kuwapo kwa mazungumzo ya aina hiyo na kusema kupitia tafiti mbalimbali taifa hili litaenda mbele katika kujenga uchumi wa viwanda.

  Mkutano huo unaohusisha washiriki mbalimbali wa ngazi za juu wa biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China umeitwa kama sehemu ya mchango wa ESRF katika ujenzi wa uchumi wa viwanda wa Tanzania.

  “Sisi serikalini tunaridhishwa na juhudi zinazofanywa na taasisi za kitafiti kama hii zenye lengo la kusaidia juhudi za serikali za kuhudumia watu wake na kuongeza ustawi” alisema Mpango.

  Soma Zaidi


  Last updated on 2017-07-18
ESRFs activities are supported by the Government of the United Republic of Tanzania, United Nations Development Programme (UNDP), African Capacity Building Foundation (ACBF) and International Development Research Centre (IDRC)