ESRF Yafanikisha Mkutano wa 5 wa Mwaka, Wajadili Uchumi.

  Imeleezwa kuwa ili kumwezesha kila mwananchi wa Tanzania kupata maendeleo na kuondokana na janga la umaskini, Serikali haina budi kutunga sera ambazo zitamgusa kila mwananchi na kuwa na faida jambo ambalo litawasadia kukuza uchumi wao binafasi na taifa kwa ujumla.

  Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Ashatu Kijaji akihutubia katika mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF) jijini Dar es Salaam.(Picha na Said Khalfan wa KVS Blog)

  Hayo yamesemwa katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Philemon Luhanjo katika mkutano wa siku moja wa kujadili sera za kijamii zinavyoweza kusaidia kubadilisha uchumi wa Tanzania, mkutano ambao uliandaliwa na ESRF.

  Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini wa ESRF, Philemon Luhanjo, akizungumza katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania ulioandaliwa na ESRF.

  Luhanjo alisema ni vyema Serikali inapokuwa inatunga sera ihakikishe zinakuwa na faida kwa wananchi ili ziweze kuwasaidia kupata maendeleo na kuboresha maisha yao na hata wakati nchi ikielekea katika uchumi wa kati kila mwananchi ahusike na mabadiliko hayo.

  “Sera zipo nyingi, zipo za maendeleo ya jumla, elimu, afya, kilimo, viwanda na kila kitu, sisi tunajaribu kuangalia tunapotengeneza sera mbalimbali tuhakikishe kwamba sera hizo zitamnufaisha binadamu, kwamba chochote unachofanya kiwe nikwa faida ya mwanadamu, mipango na malengo yote yawe yanamlenga binadamu kuondoa matatizo yake,

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akitoa maelezo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi katika mkutano huo.

  Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, Amon Manyama akizungumza katika mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.

  Mtafiti mshiriki mwandamizi wa ESRF, na mashauri wa ufundi wa mradi wa THDR Profesa Marc Wuyts, akiwasilisha mada Situating social policy transformation: A conceptual framework, kwenye mkutano wa tano wa mwaka wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania.

  Mchokoza mada kutoka taasisi ya Daima na Mtafiti mwandamizi mshiriki ESRF, Profesa Samwel Wangwe, akitoa maelezo yake kuhusu mada iliyowasilishwa mezani kwa wajumbe.

  Wageni waalikwa wakifuatilia mada mbalimbali kwa makini katika mkutano wa tano wa mwaka wa ESRF wa kujadili sera za jamii na mahusiano yake kwenye mabadiliko ya kiuchumi nchini Tanzania

  Soma Zaidi


  Last updated on 2016-11-30
ESRFs activities are supported by the Government of the United Republic of Tanzania, United Nations Development Programme (UNDP), African Capacity Building Foundation (ACBF) and International Development Research Centre (IDRC)