Vijana Wahimizwa Kujishughulisha Kuleta Tija.

  TABIA ya vijana kutojishughulisha katika miradi mbalimbali yenye tija kumeeelezwa kuwa moja ya vyanzo vya kudorora kwa uchumi.

  Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama katika ufunguzi wa kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika katika ukumbi wa shule ya msingi Allience Mjini Bariadi. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama akitoa hotuba ya ufunguzi wa kongamano la vijana Simiyu lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

  Alisema kumeanza kujitokeza hali ambapo vijana nchini kutokupenda kujishughulisha katika miradi mbalimbali ya kiuchumi na hivyo kushindwa kuondokana na umaskini na pia kuchangia katika pato la taifa. Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza machache awali kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama kufungua kongamano la kitaifa la vijana lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

  Alisema kuwa vijana wanaongoza kwa idadi kubwa lakini wanashindwa kujishughulisha kuhakikisha wanapata maendeleo ambayo yanaweza kulisaidia taifa. Meza kuu mgeni rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama, Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Vijana, Wazee, Wanawake na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Moudline Castico (wa tatu kulia), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Simiyu Dk.Titus Kamani ( wa pili kulia), Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Amon Manyama (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida (kushoto), Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Bunge, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh. Anthony Mavunde (wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa tatu kushoto).

  Mhagama alisema katika Kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Mkoa wa Simiyu, kuratibiwa na Taasisi ya utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), kwamba kuna fursa nyingi lakini vijana wanakuwa wagumu kuzichangamkia na matokeo yake kubaki wakiilalamika serikali kuwa haiwajali.

  Alibainisha kuwa serikali itaendelea kusaidia makundi ya vijana yanaoonesha nia ya kujiendeleza Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dk. Tausi Kida akiwasilisha mada ya mageuzi ya kiuchumi yanayohitajika kuboresha maisha ya vijana pamoja na hali ya uchumi nchini kwa makundi ya vijana kutoka maeneo mbalimbali nchini walioshiriki kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

  Aidha alifafanua kuwa itawaongezea mtaji wa shilingi milioni 30 kwa kikundi cha vijana cwalioanzisha kiwanda Maziwa cha Meatu pamoja na kile cha Chaki kutokana na jitihada zao walizofanya na matunda kuonekana. Mkuu wa Programu, Shirika la Maendeleo UNDP, Amon Manyama akizungumzia mchango wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa (UN/UNDP) katika Maendeleo Endelevu ya Vijana wakati wa kongamano la vijana Simiyu, lililofanyika jana katika ukumbi wa shule ya msingi Allience mjini Bariadi.

  Awali kabla ya kumkaribisha mgeni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka alisema lengo la serikali mkoani hapa ni kuhakikisha linainua pato la mkoa na kuchangia katika pato la taifa kwa kuwawezesha vijana wake kutengeneza bidhaa zinazotokana na malighafi zinazozalishwa mkoani hapa.

  Soma Zaidi


  Last updated on 2016-11-08
ESRFs activities are supported by the Government of the United Republic of Tanzania, United Nations Development Programme (UNDP), African Capacity Building Foundation (ACBF) and International Development Research Centre (IDRC)