Warsha Kuhusu Fursa Mpya za Kilimo Biashara.

    Tarehe 02 Mwezi wa 4 2016,Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) iliandaa warsha ya siku moja kuhusu fursa mpya za KILIMO BIASHARA iliyofanyika ESRF. Mkuruguenzi wa ESRF, Dkt. Tausi M. Kida akifungua warsha ya fursa mpya za kilimo biashara

    Kufuatia ESRF kushiriki katika kampeini ya Malkia wa Nguvu iliyoandaliawa na Clouds Media, kumekuwepo na muitikio mkubwa kutoka kwa wananchi kutaka kufahamu zaidi kuhusu fursa zinazopatikana katika kilimo biashara. Bi. Margareth Nzuki, Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu akiwasilisha malengo ya warsha

    Kwa kutambua hilo ESRF imefanya Warsha hii kwa lengo la kutambulisha na kuelimisha zaidi wananchi kuhusu fursa mpya za kibiashara ambazo zinapatikana katika sekta ya Kilimo.

    Picha zaidi


    Last updated on 2016-04-02
ESRFs activities are supported by the Government of the United Republic of Tanzania, United Nations Development Programme (UNDP), African Capacity Building Foundation (ACBF) and International Development Research Centre (IDRC)