Ubadhirifu Kikwazo cha Ushirika Kushamiri.

  Imeelezwa kuwa matatizo ya uendeshaji wa vyama vya ushirika hasa ya kutokuzingatiwa kwa sheria na kanuni za ushirika, wizi na ubadhirifu wa mali yamedhoofisha sana ushirika Mkoani Mwanza.

  Hayo yamesema na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Manju Msambya kwenye ufunguzi wa Mafunzo ya Uimarishaji wa Ushirika wa Akiba na Mikopo, Mwanza.

  Alisema kutokana na ukweli huo ni vyema vyama vya ushirika vikawa makini katika uchaguzi na kuhakikisha kwamba kila wanapofanya uchaguzi wanachagua viongozi wazuri wenye uchungu na maendeleo ya ushirika na siyo wanaotanguliza maslahi yao binafsi na kupuuza ya wengi.

  Tusaidiane kupambana na maovu na kujenga ushirika ulio imara.” Alisema.

  Alisema pamoja na changamoto za kiuongozi Mwanza kwa sasa imepiga hatua kubwa upande wa SACCOS na VICOBA.

  Soma Zaidi kutipia viunganishi vifuatavyo

  Dewji Blog

  Issa Michuzi

  Michuzi Jr

  Fridaysimbaya

  Luke Music Factory

  Josephat Lukaza

  Full Shangwe

  Pamoja

  Swahili Villa

  Khalfan Said

  Rweyunga

  Othman Michuzi

  Wazalendo25

  Rweyemu Info


  Last updated on 2018-08-31
ESRFs activities are supported by the Government of the United Republic of Tanzania, United Nations Development Programme (UNDP), African Capacity Building Foundation (ACBF) and International Development Research Centre (IDRC)