Ugeugeu na Upapara wa Kupata Fedha Unakwamisha Vijana.

  Source: Blogs

  Vijana nchini Tanzania wanatakiwa kujitambua, kuacha kuwa kigeugeu na kufanya papara ya kupata fedha kama wanataka kuendelea na kufanikiwa kibinafsi na kiuchumi.

  Kauli hiyo imetolewea jana na Meneja Ajira za Kifundi kwa vijana na Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga kwenye warsha ya wadau wa kitaifa ya kujadili suala la ajira kwa vijana Tanzania .

  Kauli yake hiyo kwa vijana hao waliojumuika katika hoteli ya DoubleTree by Hilton, Dar es salaam, ilitokana na tafiti mbalimbali zilizofanyika nchini ambazo zinaonesha kwamba vijana wengi hawana msimamo wa maisha, hawana maono, hawana malengo binafsi wala kutambua matarajio.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akifungua warsha ya vijana na ajira iliyofadhiliwa na Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC). Kushoto ni Meneja Ajira za Kifundi kwa vijana na Mratibu Kazi wa Shirika la Kimataifa la Kazi (ILO) Dk. Annmarie Kiaga na kulia ni Kiongozi Mpango wa Ukuaji na Ajira wa Taasisi wa Mpango wa Shirika la Utafiti ya Maendeleo ya Kimataifa kutoka Canada (IDRC) Dk. Arjan de Haan.

  Soma Zaidi Dewjiblog

  Rweyunga Blog

  Michuzi Blog

  Kalulunga Blog

  Pamoja Blog

  Othman Michuzi Blog

  Mjengwa Blog

  Issa Michuzi Blog

  The Habari Blog

  Full Shangwe

  Luke Music Factory Blog

  Friday Simbaya Blog

  Roberto Kanda Blog

  Habari za Jamii Blog
  Last updated on 2015-09-18
ESRFs activities are supported by the Government of the United Republic of Tanzania, United Nations Development Programme (UNDP), African Capacity Building Foundation (ACBF) and International Development Research Centre (IDRC)