Warsha ya Fursa za Ufugaji Samaki Kibiashara (Ufugaji kwa Kutumia Mabwawa, Vizimba na Matanki).

  Date: Saturday Jul 22, 2017

  Organiser: Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)-Idara ya Maarifa na Ubunifu

  Place: Ukumbi wa Mikutano - ESRF

  Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)-Idara ya Maarifa na Ubunifu ikishirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine-Idara ya Sayansi ya Wanyama, Ukuzaji Viumbe maji na Nyanda za malisho, Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) - kikosi cha kambi ya Rwamkoma pamoja na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), inaandaa warsha ya siku moja kuhusu fursa za ufugaji samaki kibiashara kwa kutumia mabwawa, vizimba na matanki itakayofanyika tarehe 22/7/2017 siku ya Jumamosi katika Ukumbi wa mikutano wa ESRF kuanzia saa mbili na nusu (2:30) asubuhi.

  Kutokana na tafiti zilizofanywa, imedhihirika kwamba, wananchi wengi wamekuwa na muitikio na hamasa ya ufugaji samaki kibiashara. Kwa kulitambua hilo ESRF ikishirikiana na taasisi zilizotajwa hapo juu, imeandaa mada mbalimbali zitakazowasilishwa na wakufunzi waliobobea katika ufugaji wa samaki. Mada hizo zinajumuisha:-

   

  MADA

  MWASILISHAJI

  TAASISI

  1

  Ufugaji samaki katika mabwawa (pond fish farming),

  Emmanuel Maneno

  Kituo Cha Ufugaji Samaki Mbegani - Idara Ya Ukuzaji Viumbe Majini

  Nkhumbo Kantena (Mfugaji Kibiashara Mzoefu)


  RUVU FARM

  2

  Ufugaji  samaki katika vizimba (cage fish farming),

  Ltn. Kelvin Ngondo

  JKT

  3

  Ufugaji samaki katika matanki (Recirculating Aquaculture System-RAS)

  Ltn. Joseph Lyakurwa

  JKT

  4

  Uandaaji wa vyakula na malisho ya samaki

  Dkt. Nazael Madalla

  SUA

  5

  Masoko (Market Linkages)

  ESRF

  ESRF

  Watakaopenda kuhudhuria wanatakiwa kuthibitisha ushiriki wao kabla ya tarehe 21/7/2017 saa 5 asubuhi kwa kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kupitia namba: 0626 645 245 au kujisajili kupitia
  Last updated on 2017-07-20
ESRFs activities are supported by the Government of the United Republic of Tanzania, United Nations Development Programme (UNDP), African Capacity Building Foundation (ACBF) and International Development Research Centre (IDRC)